Bw. Patience Ntwina
Wasifu
Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora
Wakili wa Serikali Mkuu na Mwendesha Mashtaka ya jinai kwa miaka kumi na tatu. Shughuli hizo zilihusisha kusimamia ukusanyaji wa ushahidi kwa kuelekeza vyombo vinavyohusika na upelelezi wa makosa ya jinai; kuandika maoni ya kisheria; kuandaa hati za mashtaka; kuendesha kesi Mahakama ya Wilaya, Mahakama ya Hakimu Mkazi na Mahakama Kuu. Vile vile kusimamia uendeshaji wa kesi za jinai ngazi ya rufaa katika Mahakama ya Rufani. Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Katiba na Sheria na kushughulika na masuala ya uratibu wa utoaji wa huduma ya msaada wa kisheria na baadaye katika nafasi ya Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na Ufuatiliaji Haki iliyokuwa na jukumu la kusimamia na kuratibu mabadiliko ya Katiba ya nchi na maboresho ya mifumo ya haki jinai nchini kwa kipindi cha miaka tisa.
Na sasa katika nafasi ya Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na majukumu ya kusimamia shughuli na uendeshaji wa Tume na kuratibu masuala yanayohusu Tume kwa ujumla.