Kitengo cha Ununuzi na Ugavi
Kitengo cha Ununuzi na Ugavi
- Kusimamia ununuzi wowote na uuzaji wa mali za Tume kwa njia ya Zabuni isipokuwa usuluhishi na kutunuku zabuni;
- Kuratibu shughuli za Bodi ya Zabuni ya Tume
- Kutekeleza maamuzi ya Bodi ya Zabuni ya Tume;
- Kufanya kazi kama Sekritarieti ya Bodi ya Zabuni ya Tume
- Kuandaa mpango wa Ununuzi na Uuzaji wa mali za Tume kwa njia ya zabuni;
- Kupendekeza ununuzi na uondoshaji wa mali za Tume kwa utaratibu wa zabuni;
- Kupokea na kukusanya upungufu wa mahitaji kutika katika idara, vitengo na ofisi za matawi na kushauri kuhusu mahitaji hayo;
- Kuandaa nyaraka za zabuni kwa ajili wazabuni kushiriki;
- Kuandaa matangozo ya fursa za zabuni; Kuandaa rasmu za Mikataba;
- Kutoa mikataba iliyothibitishwa na kusainiwa;
- Kuandaa na kuhifadhi kumbukumbu za mchakato wa ununuzi na uuzaji wa mali za Tume;
- Kuandaa na kutunza orodha au kitabu cha mikataba yote ambayo Tume imetunuku;
- Kuratibu kazi za ununuzi na uondoshaji wa mali za serikali katika ofisi zote za Tume; na
- Kuandaa taarifa nyinginezo kadri zitakavyo hitajika muda wowote.