ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

ELIMU YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA YA WAFIKIA SHULE YA TUMATI

24 Mar, 2025
ELIMU YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA YA WAFIKIA SHULE YA TUMATI

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora hufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa haki mbalimbali  kuhakikisha haki za binadamu zinatunza na kuhifadhiwa nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi, Idara ya elimu kwa Umma ,Mawasiliano ,Tafiti na Nyaraka, Bi.Monica Mnanka  wakati wa utoaji wa elimu ya haki za binadamu na utawala bora kwa  wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Tumati Katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu leo Machi, 2023

Aidha, Bi.Mnanka amesema kuwa  Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imeanzishwa na Serikali ikiwa na  jukumu kubwa la kulinda na kuhifadhi haki za binadamu nchini ili kuepuka uvunjifu wa haki hizo.

“Serikali ndio mdau wa kwanza wa kulinda haki za binadamu nchini kutokana na kuwa na majukumu mengi imeanzisha Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ili iweze kulinda haki hizo” amesema Bi.Monica

Bi.Monica ameongeza kuwa THBUB pia hufanya  tafiti mbalimbali katika kuangalia haki hizo zinapatikana kwa kila mtu ,usawa na kwa wakati.

“Moja ya tafiti iliyofanyika hivi karibuni ni kuhusu upatikanaji wa haki ya afya  nchini katika nyanja mbalimbali “amesema Bi.Mnanka

Pia Bi Monica ametoa wito kwa wanafunzi hao kujiepusha na matumizi mabaya ya Mitandao ya Kijamii  ili waweze kutimiza haki yao ya kupata elimu