Haki Sports Washiriki SHIMIWI
Watumishi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) wameshiriki katika ufunguzi wa Mashindano yanayoandaliwa na Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) yanayoendelea Mkoani Morogoro.
Mashindano hayo yamefunguliwa rasmi na Naibu waziri Mkuu na waziri wa Nishati Mhe.Dkt. Dotto Mashaka Biteko (Mb) Septemba 25, 2024
Mhe. Dkt. Biteko amesema kuwa watumishi wa umma ni vyema kushiriki katika michezo hiyo kwani inasaidia kuwakumbusha na kubadilishana uzoefu, maarifa na kujifunza kwa taasisi zinazofanya vizuri katika kutekekeleza majukumu yao ya kuwahudumia wananchi bila kujali hali zao.
“Mmekuja kushiriki katika michezo lakini pia, mtatumia muda huu kubadilishana uzoefu ili kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi na kuongeza juhudi katika utendaji kazi”amesema
Mhe.Dkt. Biteko
Pia, alisisitiza umuhimu wa watumishi Kushiriki katika zoezi linaloendelea la uandikishaji katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura.
“Natumai kuwa wote mnafahamu kuwa mwaka huu kuna uchaguzi wa serikali za mitaa,nichukue nafasi hii kuwasisitiza kushirki kikamilifu katika zoezi hilo ili mtimize haki yenu ya kikatiba”amesema
Mashindano hayo yameanza tangu 19 Septemba 2024 na yanatarajia kumalizika 05, Oktoba 2024
Timu ya Haki Sports imeshiriki katika michezo ya Uvutaji Kamba wanawake na wanaume, mpira wa Pete, Riadha na michezo ya jadi. Ambapo timu ya Uvutaji kamba wanaume imefanikiwa kuingia katika hatua ya 16 bora inayotarajiwa kuchezwa Septemba 27 asubhi na timu kutoka Wizara ya Mifugo.