Hakisports washiriki Ufunguzi wa SHIMIWI Iringa
Oktoba 4,2023 Wanamimchezo wa Hakisports wameshiriki ufunguzi wa Mashindano ya Shirikisho la Michezo la Wizara na Idara za Serikali(SHIMIWI) yaliyofanyika Viwanja vya Samora,Mkoani Iringa.
Mgeni rasmi wa ufunguzi wa Mashindano hayo ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri Nishati Mhe. Dkt.Doto Biteko Kwa Niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan.
Aidha Mhe. Dkt Biteko amewahimiza Watanzania ikiwemo wanamichezo wanaoshiriki mashindan ya 37 ya Shirikisho la Michezo la Wizara na Idara za Serikali(SHIMIWI) kuhakikisha kuwa na mpango maalum wa kuendelea na michezo mahali pa kazi ili iwe tija na uwajibika kwa wafanyakazi.
Mhe Dkt Biteko ametoa wito kwa waajiri kutoa fursa kwa wafanyakazi kushiriki mashindano hayo kwani yana lengo la kuwakutanisha Watumishi mbalimbali kutoka Wizara na taasisi za Serikali kufahamiana.
“Nawaasa sana wafanyakazi kujituma kwa bidii na kushiriki michezo ili kujiepusha na maradhi pamoja na kuweka mashirikiano baina ya Wizara na taasisi kpiti mashindano hayo”.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bw.Patience Ntwina amewapongeza wanamichezo wa Hakisports kwa kufanya vizuri katika michezo iliyopita
“Naamini kupitia michezo hiyo mtajipanga vyema katika mashindano yajayo”alisema Bw.Ntwina
Mashindano ya Shirikisho la Michezo la Wizara na Idara za Serikali(SHIMIWI) yalianza tarehe 27 Septemba,2023 Mkoani na kutarajia kumalizikia Oktoba14,2023.