Kamishna THBUB atoa taarifa kuhusu ukusanyaji wa Maoni Zanzibar
WADAU mbalimbali wametakiwa kutoamaoni yao ili kusaidia uandaaji wa
mpangokazi wa kitaifa wa haki zabinadamu na biashara.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya Habari kuhusiana na zoezi la ukusanyaji wa maoni
hayo huko Rahaleo Mjinu Unguja Kamishna Tume ya haki za binaadamu na Utawala
Bora Tanzania Mhe.Khatib Mwinyichande alisema tume inatarajia kuendesha zoezi laukusanyaji wa maoni ya wadau kuanzia julai 29 hadi agosti 2mwaka 2024 ili kupata taarifa muhimuzitakazosaidia kupatikana mpango shirikishiwa tume hiyo.
Alifahamisha kuwa Serikali zote mbili zipokwenye Maandalizi ya Mpango kazi wa
kitaifa wa haki za binaadamu , hivyo wadauwana mchango mkubwa katika kufanikisha
upatikanaji wa mpango huo.
Alieleza kuwa zoezi hilo litawafikia wadauwa utalii, uchumi wa buluu na nishati katika
maeneo mbalimbali ya mikoa ya Zanzibarbaada ya kukamilika kwa zoezi kama hilo
Tanzaniabara .
Aidha alisema tume imepanga kuwafikiamamlaka ya uhifadhi na utekelezaji wa Mji
Mkongwe,kamisheni ya Utalii Zanzibar,umoja wa hoteli (HAZ), umoja wawawekezaji wa utalii(ZATI) , umoja wawaongoza utalii (ZATOGA),umoja wawaendesha utalii (ZATO),mamlaka yakukuza uwekezaji (ZIPA) pamoja na
Mamlaka za mapato Tanzania na Zanzibarndani ya Mkoa wa Mjini magharibi.
Vilevile alisema julai 31,2024 Tumeinatarajia kufanya mikutano na baadhi yawafanyakazi wa hoteli za kitalii zilizopoNungwi na Kendwa na wananchi wanaoishi
pembezoni mwa hoteli hizo pamoja nakuzungumza wananchi wanaoishi eneo la
uchimaji mchanga Donge Chechele ilikupata maoni yao.
Alifahamisha kuwa julai 29 ,2024 tume imepanga kukutana na wananchi wanaoishi
karibu na eneo la uchimbaji na uchakatajiwa matofali ya kifusi Vitongoji Mkoa wa
Kaskazini Pemba.Kamishna huyo aliwataja wadau wa uchumi
wa buluu wanaotarajiwa kufikiwa kuwa nipamoja na Mamlaka ya kusimamia Uvuvi
wa Bahari kuu, Shirika la Biashara laZanzibar (ZSTC) shirika lameli na bandari, kampuni ya mwani,wakulimana na wafanyabiashara wamwani,pamoja na wafanyabiashara wa
samaki katika maeneo mbali ya MjiniMagharibi, kusini unguja,kusini naKaskazini Pemba .
Hatahivyo alieleza kuwa zoezi hilolitafanyika kwa ushirikiano na wajumbe
walioteuliwa na Waziri wa Katiba na Sheriawa jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kutoka katika taasisi za Serikali na binafsipamoja na asasi za kiraia kutoka Tanzania
bara na Zanzibar.
Tume ya haki za binaadamu na UtawalaBora (THBUB) ni chombo chenye jukumu la
kuhamasisha hifadhi ya haki za binaadamuna uzingatiwaji wa misingi ya Utawala Bora
kama majukumu yake yalivyoainshwakatika ibara 130(1)(a)-(h) ya katiba ya
Jamhuri ya muungano wa Tanzania 1977na sheria ya tume ya hakiza binaadamu na Utawala Bora Sura ya391 ya mwaka 2021 kifungu cha 6.