ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

Maadhimisho ya wiki ya Sheria Nchini

03 Feb, 2023
Maadhimisho ya wiki ya Sheria Nchini

1. Katika kuadhimisha Wiki ya Sheria nchini, Mahakama ya Tanzania kwa kushirikiana na wadau wake ndani ya sekta ya Sheria iliandaa programu maalumu ya kutoa elimu kwa umma katika maeneo mbalimbali Jijini Dodoma kuanzia tarehe 22 hadi 29 Januari, 2022.

2. Lengo la programu hiyo ni kuhamasisha jamii kuhusu masuala mbalimbali ya sheria na haki za binadamu ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ambayo ni *"Umuhimu wa wa Utatuzi wa Migogoro kwa Njia ya Usuluhishi katika Kukuza Uchumi Endelevu: Wajibu wa Mahakama na Wadau*"

3. Maeneo yaliyotembelewa ni Soko la Sabasaba na Machinga, Mwangaza fm, Dodoma fm, Shule ya Msingi Chang'ombe, Shule ya Msingi Uhuru, Shule ya Sekondari ya Wasichana Msalato, Shule ya Sekondari Wela, Kituo cha Polisi Kati, Gereza Kuu la Isanga, Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini, na Hospitali ya General.

4. Wadau walioshiriki katika programu hiyo ni Mahakama ya Tanzania, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Jeshi la Polisi Tanzania, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Tume ya Usuluhishi na Uamuzi, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Uhamiaji, Baraza la Ardhi, Idara ya Ustawi wa Jamii Mkoa, Chama cha Wanasheria Tanganyika na  Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania.

5. Makundi yaliyofikiwa ni Wanafunzi, Walimu, Maafisa wa Jeshi la Polisi, Wafanyabiashara,  Wafungwa na Mahabusu, Madaktari na Wauguzi na wananchi mbalimbali.

 

 

 

Pichani:

Timu ya utoaji elimu ikikaribishwa baada ya kuwasili katika Ukumbi wa Mikutano katika Kituo cha Polisi cha Kati kwa lengo la kutoa elimu Jijini Dodoma tarehe 24 Januari, 2023 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya ya Wiki ya Sheria.