Mkutano wa Kujadili taarifa ya Itifaki ya Maputo(Maputo Protocal) iliyoandaliwa na PATHFINDER Kushirikiana na TAWLA
Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mhe.Dkt Thomas Masanja amelipongeza Shirika lisilo la Kiserikali Pathfinder na TAWLA kwakuandaa taarifa ya utafiti kuhusu Ibara za Itifaki ya Maputo(Maputo Protocal) iliyojadiliwa Agosti 31,2022 katika Ukumbi wa Nashera Hotel ulipo Jijini Dodoma.
Mhe. Masanja alitoa pongezi hizo wakati wakufunga kikao cha kujadili taarifa hiyo iliyo wasilishwa na Dr. Kalekwa Mtaalamu kutoka Shule ya Sheria(LAW SCHOOL).
Aidha Mhe.Dkt Masanja alitoa rai kwa wadau hao kushirikisha wadau wengi wanahusika na masuala ya haki za wanawake ili kufikia lengo la utafiti huo.
“Niwapongeze kwa majadiliano mazuri,ni muda muwafaka sasa wakushirikisha wadau wengine kuongeza wigo wakupokea mawazo tofauti kuhusu haki za wanawake”Alisema Mhe. Dkt Masanja
Kwa upande wake Bw.Meshack Mollel Meneja mradi Pathfinder aliwashukuru wajumbe kwakuhudhuria kikao hicho na kutoa mawazo yao kupitia taarifa iliyowasilishwa na kuahidi kufanyia kazi michango yote iliyotolewa na wajumbe wa kikao hicho.
Kikao hicho kilihudhuriwa na Wakurugenzi kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora,Maafisa wengine wa Tume, Meneja Mradi na Afisa Mradi kutoka Pathfinder, na Mratibu kutoka TAWLA.