PSC YAWATAKA WATUMISHI WA THBUB KUJUA SHERIA NA KANUNI ZA UTUMISHI WA UMMA
Wakaguzi kutoka Tume ya Utumishi wa Umma (Tanzania Public Service Commission - PSC) wamewataka Watumishi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kusoma Sheria, Kanuni na Taratibu za utumishi wa umma ili kujua haki na wajibu wao.
Rai hiyo imetolewa leo (Agosti 17, 2023) Makao Makuu ya Ofisi za THBUB jijini Dodoma wakati Wakaguzi hao wakiwasilisha taarifa yao ya awali ya ukaguzi mbele ya Menejimenti ya THBUB.
Wakaguzi hao walisema kuwa Mtumishi akizijua haki zake itamwia rahisi kuzidai pindi anapozikosa.
Ukaguzi huo ulioanza Agosti 14, 2023 ulilenga kuangalia uzingatiwaji wa Sheria, Kanuni na Taratibu za usimamizi wa Rasilimali watu katika Taasisi.
Bwana Hussein Mzee Mussa ndiye aliyeongoza Timu ya watu watatu katika ukaguzi huo. Maafisa wengine alioambatana nao walikuwa Bi. Sheila Nampera na Bi. Juliana Kombe.