THBUB YAACHA TABASAMU ARUSHA

Katika kuelekea Siku ya Wanawake Duniani Wanawake wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) wameachia tabasabu kwa Watoto wa kituo cha kulelea Watoto waishio katika mazingira magumu cha Matonyok kwa kutoa msaada baada ya kutembelea katika Kituo hicho machi 6, 2025.
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo Kamishna wa THBUB Mhe. Amina Talib Ali amewapongeza waanzilishi na walimu wa kituo hicho kwa kutoa huduma ya malezi na elimu kwa Watoto waishio katika mazingira magumu na wenye ulemavu.
Mhe. Amina amesema kuwa Wanawake wa THBUB wameguswa na kuamua kutoa msaada huo kwa kuwa wanatambua mchango unaofanywa na Familia hiyo.
“Tume inakupongeza Sana wewe na Familia yako kwa kuliona hili la kuhudumia Watoto wenye uhitaji, Wanawake wengi wanatelekeza Watoto kwa sababu ya kukosa uvumilivu wa kuhudumia Watoto wenye mahitaji maalumu” amesema Mhe. Amina.
Naye Mkurugenzi wa kituo hicho Bi. Emmy Nicholaus Sitayo amesema Kituo hicho kinahudumia wanafunzi Hamsini na nane ambapo wasichana ni Thelathini na wavulana wakiwa ishirini na nane.
Bi. Sitiya ameongeza kuwa kituo hicho kilianzishwa kwa lengo la kupunguza vitendo vya ukatili vinavyofanyiwa baadhi ya Watoto yatima na waishio mitaani ikiwemo ubakaji, kupigwa na kunyimwa haki za msingi za binadamu.
“Nashukuru sana kwa ujio wenu katika Kituo hiki na msaada mlio utoa kwa ajili ya Watoto hawa, kwani mmefanya jambo kubwa sana la kuwafanya wwajisikie kuwa ni kundi linalo thaminika katika jamii. Tunaomba Muendeleze Moyo huo wa Upendo kwa Watoto wenye uhitaji amesema Bi Sitiya.
i.