ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

THBUB YAITAKA JAMII KUTAMBUA KUWA WANAWAKE WANA HAKI SAWA NA WANAUME KATIKA KUMILIKI MA

09 Mar, 2025
THBUB YAITAKA JAMII KUTAMBUA KUWA WANAWAKE WANA HAKI SAWA NA WANAUME KATIKA KUMILIKI MA


Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Malalamiko na Uchunguzi Bi. Suzana Ndeona (THBUB) alipokuwa akitoa elimu ya haki za binadamu na misingi ya utawala bora katika banda la THBUB lililopo katika maonesho ya taasisi za serikali na binafsi kuelekea maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake.
 
Bi. Ndeona amewaeleza kuwa Sheria za Tanzania zinaruhusu na kutambua mwanamke kumiliki na kurithi mali lakini bado kumekuwa na changamoto katika utekelezaji wake kutokana na kuwepo kwa mila na desturi potofu na kandamizi kwa wanawake.
Pia Bi. Ndeona ameongeza kuwa bado wanawake wengi wana uelewa mdogo kuhusu haki zao kisheria.


“Ni muhimu sisi wanawake tukatambua kuwa tuna haki sawa na wanaume katika kumiliki mali ikiwemo mashamba, nyumba na hata kurithi mali kama wanavyofanya wanaume. Kujua haki yako inasaidia kufikia usawa wa kijinsia na maendeleo endelevu” Amesema Bi Ndeona.
Wanawake wanapaswa  kujithamini na kutambua kuwa mali hazina jinsia hivyo tunapaswa kutumia fursa zilizopo katika kujiendeleza na kujikomboa kiuchumi.