THBUB yakutana na wadau wa Makampuni ya Simu
Septemba 20, 2024, ujumbe wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) ukiongozwa na Kamishna Nyanda Shuli ulikutana na wawakilishi wa Makampuni ya Simu ya Vodacom na Airtel kwa ajili ya kujadiliana na kuweka mikakati ya pamoja itakayohuisha ushirikiano baina ya THBUB na makampuni hayo ya simu katika kuimarisha hifadhi na ulinzi wa haki za binadamu kupitia teknolojia ya mawasiliano ya simu.
Aidha, katika kikao hicho Kampuni ya Simu ya Vodacom iliwakilishwa na Bw. James Wawenje, Meneja wa Kampuni ya Simu ya Vodacom (Physical Security and LEA Security) na Kampuni ya Simu ya Airtel iliwakilishwa na Bw. Nzagi Herman, Afisa Sheria wa Kampuni ya Simu ya Airtel Tanzania. Wawakilishi wa makampuni hayo waliishukuru THBUB kwa kuwashirikisha katika kuongeza ufanisi wa uetekelezaji wa majukumu yake na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano.