THBUB YATEMBELEA MTANDAO WA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU TANZANIA*
27 Aug, 2021
LEO Alhamisi (Agosti 26, 2021) Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) Ofisi ya Dar es Salaam ilitembelea Asasi ya Kiraia ya Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) na kufanya mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali.
Mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha mashirikiano baina ya taasisi hizo mbili na kuboresha utendaji kazi.
Pia yalilenga kuimarisha masuala ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini.
THBUB na THRDC zina makubaliano ya kufanya kazi pamoja tangu mwaka 2018.
Ziara hiyo ya Siku moja iliongozwa naKamishna Mkazi wa Kanda ya Mashariki, Mhe. Nyanda Shuli akiambatana na Bw. Francis Luziga (Afisa Uchunguzi Mkuu) na Bi. Nancy Ngula (Afisa Uchunguzi Mwandamizi).