Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora yaanza Shamrashamra za Miaka Ishirini tangu kwa kupanda miti.
Serikali imeipongeza Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwa kuhamasisha jamii kupanda na kutunza ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka ishirini tangu kwa kuanzishwa kwa Tume hiyo.
Hayo alisema Naibu Katibu Mkuu,Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu kazungu wakati wa shughuli ya kupanda miti iliyofanyika Septemba 10,2022 katika Viwanja vya Kwa Swai Jijini Dodoma.
Dkt Kazungu alisema kuwa hatua iliyochukuliwa na Tume itasaidia kukuza uelewa wa jamii juu ya wajibu wao wakupanda na kutunza miti kwa manufaa yao na Taifa kwa Ujumla.
“Napenda kutumia nafasi hii kuipongeza Tume,kwani jambo hili ni utekelezaji wa maagizo ya ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassani kuhusu umuhimu wa kutunza vyanzo vya maji na misitu na kila mtu mahali alipo kupanda miti ili kutekeleza Sera ya Taifa Uhifadhi wa Mazingira ya Mwaka 2020/21 hatua itakayotupeleka kufikia lengo tulilojiwekea katika Mkakati wa Utekelezaji wa Sera hiyo,’’alisema Dkt, Kazungu
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora,Bw.Patience Ntwina alisema kuwa eneo lililopandwa miti lina ukubwa wa hekari mbili ambapo jumla ya miche 600 inayojumisha miche ya miti ya kivuli na matunda ambayo mahususi katika eneo hilo imepandwa kwa maelekezo ya wataalamu kutoka Ofisi ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania.
‘Tume imeweka mikakati ya kutunza miti hii kwa kuweka miundombinu ya umwagiliaji kwa muda wa siku tisini(90)ambazo tunaamini itakuwa imeimarika kwa mizizi kushika udongo,aidha miti hii itakapokuwa itapunguza joto na kurekebisha hali ya hewa pamoja na kupunguza kazi ya upepo,vimbunga na kukabilianda na mmomonyoko wa udongo’’alisema Ntwina
Naye, Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mhe.Mathew P.M.Mwaimu(Jaji Mstaafu) alisema kuwa kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya haki za binadamu na mazingira naTume inatambua utekelezaji na upatikanaji wa haki mbalimbali za binadamu unategemea kwa kiasi kikubwa uwepo wa mazingira yanayowezesha haki hizo kupatikana