Tume Yaanza Ukusanyaji Wa Maoni Wa Haki Za Binadamu Na Biashara
TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inatekeleza jukumu la kukusanya maoni juu ya mpango kazi wa taifa wa haki za binadamu na biashara .
Jukumu hilo limeamza kukusanya maoni wenye viwanda na kampuni katika hatua ya kwanza kumalizika wanakwenda kwa wafanyakazi ili kuratibu mpango kazi wa Taifa.
Hayo ameyasema Kamishina wa Tume hiyo Nyanda Shuli wakati wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ofisi ya Tawi la Dar es salaam.
Amesema Tume hiyo ilipewa jukumu la kukusanya maoni kutoka kwa wadau mbalimbali kuhusiana na namna ya kulinda haki za binadamu na maeneo ya Nishati, kilimo na uchumi wa buluu,utalii, Teknolojia Uchukuzi.
Shuli amesema katika kulitekeleza hilo tume ilizingatia wajibu wa serikali katika kulinda haki za binadamu kwa kulipa fidia kwenye maeneo ambayo wananchi walitoa maeneo.
Aidha amesema Tume hiyo ilipewa jukumu la kuratibu mchakato wa uandaji wa mpango kazi wa taifa wa haki za binadamu na biashara jukumu hili tumepewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Tutakusanya maoni kupitia hizo timu za wataalamu waliosambaa maeneo mbalimbali nchini na baadhi yetu tutakuwepo kwenye ukanda huu kwa maana ya Dar es Salaam, na Pwani tukiwa na lengo la kukutana na wafanyakazi wa kampuni binafsi,lengo ikiwa ni kukutana na taasisi za serikali na wananchi wanaozunguka maeneo mbalimbali ambayo kampuni za biashara zinafanya kazi kwa kuwapa elimu pamoja na kujua ni fidia kiasi gani wapewe ili kupisha mradi husika kwani ni haki yao ya msingi," Shuli.
Amesema taarifa kwa wananchi zoezi hilo litawafikia wananchi,wafanyabiashara,sekta binafsi na serikali na tayari mchakato umeanza julai 14 na litaitimishwa Julai 22 mwaka huu,"alisema Shuli.
Hata hivyo amesema eneo la haki za binadamu na biashara ni eneo nyeti ambapo serikali imeipa taasisi hiyo dhamana yake ilikulinda haki za binadamu kwani jambo hilo linahitaji usimamizi wa umakini na bila kufanya hivyo haki za binadamu zinakuwa zinakiukwa.
"Serikali imeiamini Tume na tumefanya mchakato huo na kufanya uchambuzi wa mawazo uliotuongoza kufika hatua nyingine ambayo ni kufanya mapitio ya nyaraka zinazoangalia undani wa haki za binadamu na biashara tulichambua tupo wapi kama nchi katika uchambuzi huo kupitia mawazo ya wadau tumegundua maeneo yanayohitaji kupewa kipaumbele zaidi wakati kutengeneza mpango kazi wa Taifa "Amesema Kamishna Shuli.
Aliongeza:"maeneo yatakayowekwa kipaumbele katika mpango huo ni pamoja na nishati na uzinduaji , uzalishaji na usindikaji , kilimo na uchumi wa buluu, utalii na ukarimu , ujenzi na uchukuzi, huduma za kidigitali na mawasiliano pamoja na biashara na fedha,"alisema.
Aidha Shuli amesema Tume baada ya kuhitimisha uchambuzi huo sasa ni wakati wa hatua ya pili na timu ya wataalamu kutoka kwenye taasisi za serikali , asasi za kiraia na sekta binafsi watakusanya maoni na kuchukua taarifa juu ya maeneo yaliyoainishwa kama kipaumbele.
Amesema Tume baada ya kuhitimisha hatua hiyo itaanda rasimu ya awali ambayo itarejeshwa kwa wananchi ilikujadili kama haki zao zimezingatiwa au la kwani mpango huo umelenga kuweka utaratibu mzuri namna bora ya kulinda haki za binadamu katika biashara bila kuacha changamoto ambayo inakiuka haki za binadamu ,"alisema.