*WADAU WAKUTANA KUJADILI ITIFAKI YA MAPUTO*
23 Aug, 2023
Leo Agosti 21, 2023 Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, kwa kushirikiana na PATHFINDER na TAWLA wamewaleta pamoja wadau mbalimbali wa kutoka Mashirika yasiyo ya Kiserikali kujadili masuala yaliyobainika baada ya mapitio ya Itifaki ya Maputo.
Lengo la majadiliano hayo ya siku moja yaliyofanyika Holiday Inn hotel lilikuwa kukusanya maoni na mapendekezo ya wadau hao kwa ajili ya kuishauri Serikali.
Miongoni mwa Washiriki wa kikao hicho walikuwa ni Wajumbe kutoka TAMWA, TAWLA, LHRC, Msichana Initiative, TANLAP, AGOTA, na Engender Health.
Wengine ni kutoka UMATI, WGNRR, MST, Young and Alive Initiative, MDM, Haki Elimu, WPC-ULINGO na Pathfinder International.