ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

WANANCHI WAASWA KUTOA TAARIFA YA VITENDO VYA UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU

21 Mar, 2025
WANANCHI WAASWA KUTOA TAARIFA YA VITENDO VYA UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU

 

Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe.Mohamed Khamis Hamad ametoa wito  kwa wakazi  wa Kata ya Babati kutoa taarifa ya matukio ya kikatili  pindi yanapotokea katika maeneo yao.

 Wito huo umetolewa wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mtaa wa Mjengo Kata  ya Babati Machi 20,2025 Mkoani Manyara.

Mhe.Mohamed Hamad amesema kuwa  kumekuwa na changamoto kubwa ya Jamii kujichukulia sheria mkononi  maamuzi ambayo ambayo yanamnyima mtu haki ya kuishi.

Awali akiainisha majukumu ya THBUB, Mhe Mohamed amesema kuwa THBUB imefika katika kata hiyo kwa lengo la kutoa elimu ya haki za binadamu na utawala bora pamoja na kupokea malalamiko ya wakazi hao yanahusu uvunjifu  wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora. 
‘Niwaombe  nafasi hii muitumie vizuri kuwasilishe malalamiko yenu ili yapatiwe ufumbuzi.

Upokeaji wa malalamiko kutoka kwa wananchi  ni mojawapo wa utekelezaji wa majukumu ya Tume ambayo yameainishwa  katika ibara 130 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.