WANAWAKE THBUB WA WASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI
09 Mar, 2025

Wanawake wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) wameungana na wanawake Duniani kote katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, ambayo kitaifa yamefanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Mkoani Arusha machi 8, 2025.
Maadhimisho hayo yameongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye alikuwa mgeni Rasmi wa Maadhimisho hayo.
Katika maadhimisho hayo THBUB imehimiza Jamii kuona umuhimu wa kushirikisha Wanawake katika mipango ya maendeleo na kuhakikisha wanapata fursa na haki sawa na Wanaume.
Wanawake THBUB walishiriki katika maadhimisho hayo, yaliyoongozwa na Kauli mbiu isemayo:
"Wanawake na Wasichana 2025: Tumeimarisha Haki, usawa na Uwezeshaji