WATENDAJI WA KATA WATAKIWA KUZINGATIA HAKI NA USAWA KATIKA KUWAHUDUMIA WANANCHI

Mchunguzi Mkuu Msaidizi kutoka Tume ya Haki za Binadamu, Bw. Halfan Botea amewataka Watendaji wa Kata za Halmashauri ya Mji wa Babati kuzingatia haki, usawa, uadilifu, utawala wa kisheria, uwazi, ushirikishaji wa Wananchi wanapotimiza majukumu yao ili kujiepusha na ukiukwaji wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora.
Hayo ameyasema wakati akiwasilisha mada ya haki za binadamu na utawala bora wakati wa mafunzo kwa watendaji hao yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Mji Babati Machi 19, 2025.
Aidha amebainisha faida mbali mbali za kusimamia haki za Binadamu na Utawala Bora kuwa ni chanzo cha uwepo wa amani katika jamii na kuleta uzalishaji bora kwa Maendeleo ya jamii.
Kwa upande Watendaji Kata wakielezea umuhimu wa mafunzo hayo, wameeleza kuwa mafunzo ya haki za binadamu na utawala bora waliyoyapata yamekuwa na manufaa makubwa kwao, huku wakiahidi kuyatumia katika utekelezaji wa majukumu yao.
Aidha, Bw. Botea amebainisha faida mbali mbali za kusimamia haki za Binadamu na Utawala Bora kuwa ni pamoja na uwepo wa amani katika jamii na kuleta uzalishaji bora kwa Maendeleo ya jamii.