WAZAZI WAASWA KULINDA MAADILI YA WATOTO

Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) Mhe. Amina Talib Ali Ametoa wito kwa wazazi na walezi kutimiza jukumu lao la kulea na kulinda maadili ya Watoto kutokana na Kukithili kwa vitendo vya Uvunjifu wa maadili katika Jamii.
Kamishna Amina ametoa wito huo katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika Kata ya Kanyonza iliyopo wilayani Kakonko Mkoani Kigoma Februari 21, 2025.
Amesema kuwa wazazi na walezi wana jukumu kubwa katika kusaidia vijana kuwa na maadili mazuri na kutengeneza vyema maisha yao ya baadaye na kuwa na Taifa lenye siha Njema.
“Ni jukumu letu wazazi kuhakikisha kuwa Tunafahamu Watoto wetu wanapokwenda, muda anaotoka na kurudi nyumbani na tuna wajubu wa kukaa na kuzungumza na Watoto juu ya changamoto na vishawishi anavyovipata wakiwa Shule na hata maeneo yawayocheza ili kuhakikisha kwamba mienendo yake inakuwa salama muda wote. Amesema Mhe.
Pia Kamishna ameongeza kuwa wazazi wanapaswa kushilikiana na Taasisi zote zinazolea Watoto ikiwa ni pamoja na shule na nyumba za ibada kwani kumekuwa na tabia ya baadhi ya wazazi kufumbia macho tabia mbaya zinazofanywa na Watoto wao na kwa kigezo cha kumpenda na kuona aibu ya kuzungumza na mtoto na kuacha Taasisi hizo pekee ndizo zishughulikie maadili ya Watoto.
“Tunatakiwa kufanya kazi ya kutafuta pesa lakini pia tukumbuke kutenga muda wa kukaa na Watoto, Watoto wengi wanakatisha masomo kwa sababu ya kunyanyaswa kingono wengine kupatiwa mimba wakiwa bado wanasoma. Haya yote yanatokea kwa sababu wazazi na walezi tumesahau wajibu wetu kama walinzi na wasimamizi wa maadili ya Watoto wetu” Amesema Mhe. Amina