Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Balozi Pindi Chana ateta na Mwenyekiti wa Tume
23 Oct, 2023
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe.Balozi Dkt. Pindi Chana amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Jaji Mstaafu, Mhe. Mathew Mwaimu.
Mazungumzo yao yamefanyika leo tarehe 21 Oktoba, 2023 pembezoni mwa Kikao cha 77 cha Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kinachoendelea katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha.
Wakati huohuo, Mhe.Balozi Chana amekutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) ambao ni Kabidhi Wasii Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu Bw. Frank Kanyusi na Naibu Kabidhi Wasii, Bi.Irene Lesulie.