ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

ZIARA YA THBUB ZANZIBAR

29 Sep, 2024
ZIARA YA THBUB ZANZIBAR

Leo Septemba 26, 2024 Ujumbe wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) ukiongozwa na Katibu Mtendaji Msaidizi Bw. Juma Msafiri Karibona akiwa na Maafisa wengine kutoka THBUB umetembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib na kufanya mazungumzo na Katibu Tawala wa Mkoa huo Bw. Mohammed Ali Khamis.

Bw. Karibona ameeleza kuwa THBUB ina jukumu la kukuza na kulinda Haki za Binadamu na misingi ya Utawala Bora nchini.
“Kwa sasa THBUB imepewa jukumu la kuandaa Mpango Kazi wa Kitaifa wa Biashara na Haki za Binadamu ambapo mpaka sasa THBUB imeshafanya kazi ya kukusanya maoni katika maeneo mbalimbali ya uwekezaji hapa nchini yaani Tanzania Bara na Zanzibar hususan katika sekta ya uvuvi, Mifugo, Madini, Viwanda, Hoteli, Usafirishaji, Kilimo, Taasisi za Serikali na Binafsi”

Mhe. Mohammed Ali Khamis, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mjini Magharibi ameikaribisha THBUB katika Mkoa huo na kusema kwamba jukumu hilo ambalo THBUB  imepewa ni kubwa na la  kipekee hasa kwa kuangazia Haki za Watoto katika Biashara na namna ya kumnasua Mtoto katika Mazingira ya utumikishwaji jambo ambalo litasaidia  kulinda Haki na Ustawi wa Mtoto.

THBUB imeanza ziara yake Septemba 26, 2024 ambapo inatarajia kutembelea maeneo mbalimbali kama vile Masoko ya Samaki ya Ngalawa, Malindi, Mazizini, Uroa, Chwaka na Charawe. Pia THBUB inatarajia kutembelea kiwanda cha Maji ya Drop of Zanzibar ili kuendelea kukusanya maoni ya wadau yatakayosaidia uandaaji wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa Biashara na Haki za Binadamu, hususani katika eneo la Haki za Watoto.