Ziara ya UJumbe wa Ubalozi wa Norway THBUB
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kushirikiana na ubalozi wa Norway nchini Tanzania.
Hayo amesema Bi.Ingrid Norstein wakati alipotembelea Makao Makuu ya Ofisi za THBUB zilizopo Mtaa wa Kilimani Jijini Dodoma Oktoba 10, 2024.
Bi. Norstein amesema kuwa, kwa zaidi ya miaka sitini (60)Tanzania na Norway zimekuwa na ushirikiano mzuri kwenye maeneo ya Biashara na Siasa, pia zimekuwa zikishirikiana katika miradi mbalimbali.
Bi. Norstein aliongeza kwa kusema kuwa Norway pia iko tayari kushirikiana na THBUB katika masuala ya siasa hususani katika eneo la utawala (Governance).
Kwa upande wake Mwenyekiti wa THBUB Mhe. Mathew P. M. Mwaimu (Jaji Mstaafu) ametaja ambayo THBUB inaweza kushirikana na Ubalozi huo katika kulinda, kukuza na kuhifadhi haki za binadamu nchini, ikiwemo Kuwajengea uwezo Maafisa Uchunguzi wa THBUB ,Utekelezaji na Uandaaji wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa Biashara na Haki za Binadamu (NAP-BHR), utoaji elimu kwa umma, ufuatiliaji wa mapendekezo ya UPR (Universal Periodic Review), Hali ya Utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo endelevu hususan lengo namb.16, pamoja kuwezesha THBUB kupata vitendea kazi na Rasilimali fedha.
Aidha,Mhe.Mwaimu ameueleza ujumbe huo kuwa THBUB inatarajia kufanya uchunguzi katika Mikoa 16 ikiwa ni moja ya utekelezaji wa majukumu yake katika kulinda na kusimamia haki za binadamu.
“Chunguzi hizi tunazotegemea kuzifanya hivi karibuni ni chunguzi maalum zinazohusu matukio ya kupotea kwa watu’’ amesema Mhe. Mwaimu.
Kwa hatua nyingine Bi Norstein ametoa pongezi kwa THBUB kwa mapokezi mazuri pamoja na ukarimu walionesha.
“Asanteni sana”amesema Bi.Norstein
Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Kamishna wa THBUB Mhe. Dkt.Thomas Masanja, Katibu Mtendaji wa THBUB Bw. Patience K. Ntwina na Afisa Uchunguzi Mkuu Bw. Fadhili Muganyizi na Bw. Victor Malunde kutoka ubalozi wa Norway nchini Tanzania.