JAMII IELIMISHWE UMUHIMU WA KUTUNZA NA KUHESHIMU UTU WA BINADAMU; M/KITI WA TUME YA HAKI ZA BINADAMU
TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Nchini,imetoa wito kwa Viongozi wa Siasa Dini na Jamii kwa ujumla ,kuhusu kuelimisha jamii umuhimu wakutunza na kuheshimu utu wa binadamu.
Akiongea Ofisini kwake, Jijini Dodoma mbele ya waandishi wa vyombo mbalimbali vya Habari, Mwenyekiti wa Tume Mhe.Mathew Mwaimu (JajiMstaafu), amesema kuwa kuna umuhimu wa viongozi hao kutoa elimu hiyo itakayosaidia kuondoa matukio ya mauaji ambayo yamekuwa yakitokea katika maeneo mbalimbali ya nchi.
Jaji Mwaimu ametoa mfano wa mauaji ya Mtoto mwenye Ualbino, Asimwe Novart ambaye alichukuliwa nyumbani kwao Kamachumu Mkoani Kagera May 30, 2024 17,2024 akiwa ameuawa na kukatwa baadhi ya viungo vya mwili wake.
“Viongozi wa dini na siasa wanajukumu kubwa la kutoa elimu ambayo itasaidia jamii ijue umuhimu wa kutunza na kuheshimu utu wa binadamu wenzao”, amesema Mhe.Mwaimu
Ameongeza kuwa Serikali ione umuhimu wa kuweka nguvu katika maeneo ya mipakani hasa mikoa ya kaskazini Magharibi ambako matukio kama hayo yamekuwa yakijitokeza kwa madai hayo ya Imani za kishirikina “ati viungo vya albino vinaweza kusababisha upatikanaji wa madini kwenye migodi na pia uongozi kwa wagombea wa kisiasa
Aidha,Mhe. Mwaimu amebainisha kuwaTume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora,imekuwa ikipokea malalamiko mengi kuhusu migogoro ya Ardhi Nchini, ambapo Mkoa wa Dodoma ndio unaongoza na changamoto kubwa ikiwa kutokuwepo kwa ushirikishwaji.
“Suala la mipango miji ni zuri katika uendelezaji wa miji hasa pale watu wa ardhi wanapokuwa wanafanya upimai ni vyema wakakaa na wananchi na kuwashirikisha ili kuondokana na migogoro hiyo”.Amesema Mhe.Mwaimu
Katika hatua nyingine,Mhe Mwaimu amesema kuwa Tume pia imepokea malalamiko ya watumishi wa Umma katika upande wa ucheleweshwaji wa mafao kwa wastaafu,mapunjo ya mshahara pamoja na Kikokotoo.