ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

THBUB yakutanisha Wadau wa watoto kujadili Mpango kazi wa Kitaifa wa Haki za Binadamu na Biashara eneo la Haki ya Mtoto

29 Oct, 2024
THBUB yakutanisha Wadau  wa watoto kujadili Mpango kazi wa Kitaifa wa Haki za Binadamu na Biashara eneo la Haki ya Mtoto

Serikali kuendelea kuweka mifumo ya kisera,sheria na taratibu kuhakiki ulinzi wa haki za mtoto kwa  ujumla  kama ilivyotamkwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 na Katiba ya Zanzibar ya Mwaka1984

Hayo amesema Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Franklin Jason Rwezimula wakati wa Mkutano wa Kitaifa wa Wadau kujadili Mpango Kazi wa Kitaifa wa Haki za Binadamu na Biashara eneo la haki ya mtoto Oktoba23, Jijini Dodoma.

"Vilevile Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeridhia mkataba mikuu kwenye mfumo wa umoja wa mataifa na mfumo wa afrika wa haki za binadamu na watu zinazolinda haki za Watoto”amesema  Dkt Rwezimula

Dkt Rwezimula aliongeza kuwa Serikali iliridhia mkataba wa umoja wa mataifa wa haki za mtoto juni 10 mwaka 1991 pamoja na kuridhia mkataba wa afrika wa haki na ustawi wa watoto machi 16 mwaka 2003,"amesema Rwezimula.

Pia Dkt Rwezimula amesema kuwa licha ya serikali ina wajibu wa msingi wa kulinda haki za binadamu kila mmoja anatakiwa kuheshimu na kulinda haki za binadamu

“Kwani Serikali imefanya jitihada kubwa kuvutia wawekezaji na shughul za biashara na kupelekea uchumi wa nchi kuendelea kukua kwa kasi kutokana na shughuli za biashara’.amesema Dkt Rwezimula

Dkt. Rwezimula  ametoa wito kwa wadao hao  kushiriki katika mdahalo kikamilifu na kuongeza kuwa mipango na mikakati maalum ya kumlinda mtoto inajumuisha mpango kazi wa kuondoa ajira mbaya ya mtoto pamoja na muongozo wa uendeshaji wa mashauri ya ulinzi wa  haki zake.

Naye Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mhe.Mathew Mwaimu(JajiMstaafu)  amesema kuwa hali ya watoto na biashara bado ni mbaya jambo lililopelekea kuingizwa katika mpango kazi wa haki za binadamu na biashara.

"Ndiyo maana tumeona wanastahili nawenyewe kuingizwa kwenye huu mpango kazi wa haki za binadamu na biashara na inafanyika hivyo kwasababu nadhani bado mnatambua kwamba watoto bado wanatumikishwa katika biashara hivyo eneo hili kufanyiwa kazi ni sehemu ya mkakati ambao utasaidia na baada ya mpango kazi huu kuandaliwa panaweza kuwa na masuala ya elimu kwa wafanyabiashara ili waweze kuona umuhimu wa kutokuajili watoto,"amesema

Awali Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bw.Patience Ntwina amesema kuwa taratibu za kuandaa Mpango Kazi wa Kitaifa wa Haki za Binadamu na Biashara, zimeanza baada ya THBUB, kukasimiwa jukumu la kutengeneza mpango huo na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya mapinduzi Zanzibar.

Aidha,Bw. Ntwina ameongeza kuwa katika kutekeleza kazi hiyo Serikali zote zilisisitiza kuzingatiwa kwa suala la ushirikishwaji Wadau na haki za makundi maalumu akiwemo mtoto.

Taratibu hizo zilifanyika kwa  kuwafikia Wadau ili kupata maoni yao ikiwa ni pamoja na; wadau wa maendeleo, Balozi; Taasisi za Kimataifa zenye hadhi za Kibalozi; Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mashirika Mwanvuli ya Biashara na Uwekezaji. Makampuni mbalimbali, Wizara za kisekta Ishirini (20) za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Wizara za Kisekta za Serikali ya Mpinduzi Zanzibar zipatazo Kumi na Nne (14); Wadau wa Biashara nchini kutoka Tanzania Bara na Zanzibar wapatao Ishirni na Tisa (29); AZAKI na vyama vya wafanyakazi (42) kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.