ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

THBUB kushirikiana na Wadau kujadili Itifaki ya Maputo,Serikali yapongezwa

23 Nov, 2023
THBUB kushirikiana na Wadau kujadili Itifaki ya Maputo,Serikali yapongezwa

Serikali inawajibu wa utekelezaji wa mikataba ya kikanda na kimataifa ambayo nchi imeridhia.

Hayo yamebainishwa na Kamishna Mkazi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala  Bora Mhe.Khatib Mwinyichande wakati wa kikao cha kujadili masuala yaliyobainika  baada ya mapitio ya Itifaki ya Maputo kilichofanyika Hotel ya Golden Tulip Zanzibar Novemba 23,2023.

Mhe.Mwinyichande ameeleza kwamba Nchi inaporidhia mikataba ya kikanda na kimataifa, inakuwa imekubali masharti yanayoendana na mikataba hiyo kwa sehemu au kwa ukamilifu wake.

 “Wajibu ambao unaendana na kuridhia mikataba hiyo ni pamoja na kuihuisha mikataba hiyo kwenye Sheria za nchi, na kutoa taarifa juu ya utekelezaji wa mkataba husika, kila baada ya kipindi fulani kulingana na matakwa ya mkataba husika”.alieleza Mhe.Mwinyichande

Aidha Mhe.Mwinyichande alieleza kuwa  Tanzania iliridhia Itifaki ya Maputo mwaka 2007 hata hivyo  haijaitungia Sheria mahsusi (domesticate) au kuwasilisha taarifa juu ya utekelezaji wa Itifaki hii.

“Nichukue fursa hii kuipongeza Serikali kwa sababu masuala mengi na ya msingi ambayo yameainishwa kwenye Itifaki ya Maputo yamezingatiwa katika sheria, sera, miongozo mbalimbali nchini na hivyo kuhakikisha kulindwa na kuheshimiwa kwa haki za wanawake kama inavyo elezwa kwenye Itifaki hiyo”. Alisema Mhe.Mwinyichande

Kwa hatua ingine Mhe.Mwinyichande alieleza kwamba Sheria ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inairuhusu Tume kuishauri Serikali iwapo kuna haja ama la, ya kufanya hivyo. Jukumu hilo limeanishwa kwenye kifungu cha 6(1) (l) cha Sheria ya hiyo, pamoja na Ibara ya 130 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Awali akieleza Mchakato wa kujadili Itifaki ya Maputo ulipoanzia Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bw,Pantience Ntwina alisema kuwa mashirikiano haya yalianza  Machi,2022 wakati wa ujumbe wa TAWLA na PATHFINDER ulipofika Tume kwa nia ya kujadiliana masuala mbalimbali ikiwemo kuhusu wajibuwa nchi kujadili katika kutekelezaji wa

 Itifaki ya Maputo.

 

Bw.Ntwina alisema kuwa kazi hii ya utafiti alipatiwa mtalam mshauri baada ya kufanya utafiti ambapo tarehe 31Agosti,2022 aliwasilisha TAWLA,PATHFINDER INTER na Tume taarifa yake ya utafiki kwenye maeneo yaliyoakisiwa na sheria sera za matamko mbalimbali pamoja na maeneo ambayo hayajaguswa.

Aidha Bw.Ntwina alisema kuwaKikao hichi ni matokeo ya ushirikiano mzuri uliopo baina ya  pathfinder,TAWLA na MARIESTOPES.

“Niwashukuru wadau hawa kwauwendelea kushirikiana nasi katika kupokea mapendekezo na maoni,Asanteni sana”alisema Bw.Ntwina

Kikao cha siku moja kilihusisha wadau mbalimbali kutoka Zanzibar wakiwemo TAMWA,PIRO,UMAT,INITIATIVES,JUMUIYA RAFIKI WANAWAKE NA WATOTO na wengine.