THBUB YATOA MSAADA WA MAHITAJI MUHIMU KATIKA KITUO CHA ALHAAFIDHU ,KONDOA
Katika kuadhimisha Siku ya Wanawake DunianiWafanya kazi Wanawake wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora wametoa msaada wa mahitaji muhimu katika Kituo cha Alhaafidhu Islamic Center kilichopo Wilayani Kondoa,Mkoani Dodoma ,Machi 7,2023.
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mhe.Amina Ali Talib alisema kuwa kila Mwaka Tume inaadhimisha kwakugusa jamii kwakuwakumbuka wenye uhitaji kwakutoa msaada.
“Maadhisho ya Mwaka huu tumeona tutembelee kituo hichi cha kulelea watoto kutoa msaada ambao tunaamini utawasaidia’’.Alisema Mhe.Amina
Aidha Bi.Amina alitoa wito kwa wanawake na watu mbalimbali kuwa na utaratibu wa kutenga kiasi kwenye kile wanachopata ili kusaidia jamii inayawazunguka hususani watu kwenye makundi mahsusi kama yatima,wajane na watoto wa mtaani.
Kwa upande wake Bi.Aisha Khalfani Nobbe ametoa shukrani kwa Uongozi wa Tume kwakutoa msaada katika kituo hicho,kwani uhitaji ni mkubwa na kuwataka waendelee kusaidia makundi mengine yenye uhitaji.